Hospitali ya Uhuru yaanza kutoa huduma

0
498

Hospitali ya Uhuru iliyopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma, imeanza kutoa huduma za matibabu kwa Wananchi wa maeneo jirani na hospitali hiyo.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt Pius Kagoma. amesema kuwa licha ya hosptali hiyo kutokamilika katika baadhi ya miundombinu, tayari wamepokea wagonjwa zaidi ya mia mbili hadi sasa.

Hospitali ya Uhuru ni moja kati ya hospitali ambazo Serikali imewekeza fedha nyingi ili iweze kuhudumia Wananchi wa mkoa wa Dodoma na maeneo jirani.