Stars yashindwa kutamba nyumbani  

0
166

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) imeshiundwa kutamba nyumbani baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja na Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
 
Kocha wa Taifa Stars Etiene Ndayiragije amewaomba Watanzania kuwa wavumilivu wakati huu ambapo timu imefanya mabadiliko ya Wachezaji wengi na kuwapa fursa vijana.
 
Mchezo huo ulikuwa sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Stars kuelekea fainali za CHAN zitakazoanza kuunguruma huko nchini Cameroon kuanzia tarehe 16  mwezi huu.
 
Katika fainali hizo, Taifa Stars imepangwa katika kundi D na timu za Zambia, Namibia na Guinea.