Simba yaachana na Kocha Sven

0
218

Uongozi wa Klabu ya Simba umetangaza rasmi kuachana na kocha wake Mkuu Sven Vandenbroeck kwa makubaliano ya pande mbili.

Taarifa rasmi kutoka Klabu hiyo zinasema kuwa nafasi ya Sven itakaimiwa kwa muda na kocha Msaidizi Selemanì Matola mpaka atakapotangazwa kocha mwingine.

Jioni ya Januari 7, 2021 kulikuwa na uvumi kuhusu kuondoka kwa kocha huyo Raia wa Ubelgiji na usiku ndipo Simba wakathibitisha rasmi kuwa kocha Sven ameondoka.

Akiwa Simba Sven Vandenbroeck ameiongoza Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho na Ngao ya Jamii na Januari 6 2021 aliiongoza kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.