Tanzania kunufaika na ugeni kutoka China

0
236


Ujio wa Waziri wa Mambo ya Nje ya China, Wang Yi nchini umetajwa kuwa na manufaa zaidi kwa Tanzania hasa katika kuboresha mahusinao ya Kidplomasia yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 50.

Akizungumza na TBC jijini Dar es salaam, Mwanadiplomasia Mwandamizi na Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Sera za Kimataifa Afrika Balozi Omary Mjenga amesema kuwa, ziara ya Waziri huyo itasaidia kuongeza fursa zaidi za kibiashara.

Amesema mwaka 2014 Tanzania na China ziliadhimisha miaka 50 ya mahusiano ya Kidiplomasia, ambapo fursa nyingi za kibiashara na uwekezaji zimeinufaisha Tanzania, na katika sekta ya elimu Wanafunzi 500 wa Kitanzania wanasoma nchini China.

Wadadisi wa masuala ya Kimataifa Wanabashiri ziara ya Waziri Wang Yi huenda ikawa inasafisha njia ya ujio wa ziara ya Pili ya Rais wa Taifa hilo Xi Jinping, baada ya ziara yake ya kwanza aliyoifanya mwezi machi mwaka 2013.

Kila mwaka Waziri wa Mambo ya Nje wa China amekuwa akifanya ziara katika nchi Tano Barani Afrika, na kwa mwaka huu ni zamu ya Nigeria, Tanzania, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Ushelisheli.