TEA yapata ugeni wa Naibu Waziri wa Elimu

0
165

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amewataka Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo ikiwemo Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) kufanya kazi kwa bidiii.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kwanza katika ofisi za TEA zilizopo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Kipanga amesema lengo la ziara hiyo ni kujiridhisha kama malengo ya Serikali yanatekelezwa kwa ufanisi kupitia Taasisi hiyo.

“Nimekuja kwenu Watumishi wenzangu ili niweze kujua utendaji wenu wa kazi unavyokwenda, nijue cha kujifunza kiweze kunisaidia katika kutoa majibu yake Bungeni”, amesema Naibu Waziri Kipanga.

Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa mazingira ya utoaji wa elimu kwa watoto wa Kitanzania yanaendelea kuboreshwa, hivyo ni muhimu kwa Taasisi mbalimbali za Serikali kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bahati Geuzye amesema kuwa, Taasisi hiyo itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Naye Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TEA, Erasmus Kipesha amesema ziara ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia katika Taasisi hiyo itaongeza ari ya kufanya kazi miongoni.mwa Watendaji.

Ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwenye Mamlaka ya Elimu Tanzania, ni ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo mwezi Desemba mwaka 2020.