Je United kuwafikia Liverpool usiku leo?

0
149

Manchester United inakutana na Aston Villa katika usiku wa mwaka mpya 2021 kwenye mchezo wake wa kiporo wa Ligi Kuu England, mchezo ukipigwa katika dimba la Old Trafford.

Endapo atashinda mchezo huo, Manchester united atafikisha alama 33 sawa na bingwa mtetezi na kinara wa ligi hiyo Liverpool wenye alama 33 baada ya kucheza mechi 16.

Aston Villa ambao wapo nafasi ya 5 wakiwa na alama 26 watakuwa na kibarua kigumu kuwazuia United kuibuka na ushindi katika mechi ya leo, huku mechi ya pili ya ligi hiyo itakuwa ni Everton dhidi ya West Ham United.