Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zuberi Ali Maulid, wakishiriki mazoezi ya pamoja ya viungo yakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Omar Hassan King, baada ya kumaliza matembezi katika viwanja vya Amaan jijini Zanzibar, wakati wa Tamasha la Kitaifa la Mazoezi ya Viungo Zanzibar lililofanyika leo.