TRA yaendelea kuvunja rekodi katika ukusanyaji mapato

0
171

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevunja rekodi kwa kukusanya mapato ya Shilingi Trilioni 2.088 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 101, katika robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2020/2021 ikilinganishwa na Shilingi Trilioni 1.664 iliyokusanywa katika robo ya kwanza iliyoishia mwezi Septemba mwaka 2020.

Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es salaam, Kamishna Mkuu wa TRA Dkt Edwin Mhede amesema, kiwango hicho cha ukusanyaji.mapato kimevuka lengo walilojiwekea la kukusanya Shilingi Trilioni 2.072.

Amewaambia Waandishi wa habari kuwa, ongezèko hilo la ukusanya mapato kwa kiasi kikubwa limechangiwa na mwamko wa Walipa kodi ambao wamekuwa wakilipa kodi zao kwa hiari.

Kwa mujibu wa Dkt Mhede, Idara ya walipa kodi wakubwa  kwa  mwezi Desemba mwaka 2020 pekee ilikusanya takribani Shilingi Trilioni Moja, Idara ya forodha ilikusanya mapato ya asilimia 97 ikikuatiwa na Idara ya walipa kodi.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, amewapongeza walipa kodi wote nchini kwa kuendelea kulipa kodi zao na ametoa onyo kwa bàadhi ya Wanyabiashara nchini ambao wamekuwa wakitoa risiti za manunuzi zisizoendana na kiwango halisi cha manunuzi.

Amesema hatua hiyo inaisababishia Serikali kukosa mapato stahiki, na kwamba Wafanyabiashara hao wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria.