Yanga kuwakosa Ntibazonkiza, Sogne na Nchimbi

0
198

Timu ya Yanga itawakosa wachezaji Sadio Ntibazonkiza, Yacoub Sogne pamoja na Ditram Nchimbi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prizons mzunguko wa pili mchezo utakaopigwa uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema wachezaji Sadio Ntibazonkiza na Yacouba Sogne waliumia wakati wa mchezo dhidi ya Ihefu lakini mchezaji Ditram Nchimbi anamatatizo ya kifamilia.

Kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Tanzania Prisons Kaze amesema wamejipanga licha ya kuwa wanakutana na timu nzuri ambayo inajua kujilinda
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli moja kwa moja mchezo ukipigwa uwanja wa Benjamin mkapa.

Michezo mingine ya leo ligi kuu Tanzania Bara Azam fc imesafiri hadi mkoani kilimanjaro ambapo watakuwa na kazi mbele ya polisi Tanzania mchezo utakaopigwa kwenye dimba la ushirika

Kocha msaidizi wa Azam Vivier Bahati amesema wameyafanyia kazi mapungufu waliyoyaona katika michezo ya nyuma ikiwemo suala la wachezaji kushindwa kumudu dakika tisini
Polisi Tanzania imeendelea kujiimarisha baada ya kumchukua mchezaji Makame Ally kutoka Yanga kwa mkataba wa miezi sita akiungana na mchezaji Kelvin Yondan aliyesajiliwa hivi karibuni

Coastal Union ya Tanga itakuwa nyumbani kuwakaribisha Namungo fc katika dimba la mkwakwani mkoani Tanga katika mchezo wa kwanza Coastal union wakiwa ugenini walifungwa goli moja kwa bila.