TAKUKURU uso kwa uso na Wakandarasi

0
214

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo, ametoa muda wa siku 14 kwa Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa nishati vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) katika mikoa mbalimbali nchini kurejesha vifaa ghali kulingana na mikataba yao.

Brigedia Jenerali Mbungo ametoa agizo hilo mkoani Iringa wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa ghali vilivorejeshwa na TAKUKURU kutoka kwa Wakandarasi 16 wa miradi ya REA vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.2.

Vifaa hivyo ni pamoja na Transforma 34 , mita 1,458 za LUKU pamoja na nyaya.