Ni United dhidi ya Manchester City nusu fainali Carabao

0
226

Manchester United itamenyana na Manchester City katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la Carabao baada ya United kuitandika Everton mabao mawili kwa bila na kutinga hatua hiyo ya nusu fainali.

Mabao ya Anthony Martial na Edinson Cavan katika dakika za lala salama za mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Goodson Park yametosha kuipeleka United nusu fainali huku mshambuliaji wake Edinson Cavan akisema sasa ni wakati wa mashetani hao kunyanyua mataji.

Nao Tottenham Hotspurs watamenyana na Brentford katika nusu fainali nyingine baada ya Spurs kuitandika Stoke City mabao matatu kwa moja katika mchezo wa nusu fainali.

Mabao ya Gareth Bale, Ben Davies na Harry Kane yameipeleka Spurs inayonolewa na Jose Mourinho katika nusu fainali na pengine sasa wanawaza kutwaa taji la kwanza wakiwa na kocha huyo Mreno.

Michezo hiyo ya nusu fainali itachezwa Januari 5 mwaka 2021.