Kunenge afanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane Tandale

0
397

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, -Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane, kukagua ujenzi wa soko la Tandale kwa lengo la kujionea kama maagizo aliyoyatoa yametekelezwa.

Miongoni mwa maagizo hayo aliyoyatoa Desemba 19 mwaka huu ni kumtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana na kuongeza idadi ya vibarua, agizo ambalo limetekelezwa.

Akiwa katika eneo hilo la soko la Tandale, Kunenge amemuelekeza Mkandarasi huyo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kabla ya mwezi Aprili mwaka 2021 na kwa ubora unaotakiwa.

Ametumia ziara hiyo kuwaagiza Wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya ujenzi mkoani Dar es salaam, kuzingatia mikataba yao kwa kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati ili iweze kutatua kero za wananchi kama ilivyokusudiwa.