Serikali kuiboresha zaidi ZBC

0
429

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid amesisitiza nidhamu na uwajibikaji ili kufanikisha malengo ya serikali katika kutoa taarifa kwa shirika la habari Zanzibar ( ZBC )

“Nasisitiza sana suala la uwajibikaji, nidhamu na uadilifu katika maeneo yetu ya kazi, ifike mahali kila mmoja anapotoka nyumbani ajue anatakiwa aje afanye nini katika eneo lake la kazi”

“Kamati (ya uchunguzi ) imeshaanza kazi rasmi, wito wangu ni kutoa mashirikiano ya moja kwa moja kwa kamati hiyo kwani ina lengo la kuboresha ZBC huku nikiamini kwamba ni kiu ya kila mmoja kuona ZBC inakuwa TV au shirika la mfano, kwahiyo ni vizuri kuandaa mikakati, ushauri na njia mbali mbali ambazo zitaiwezesha ZBC kuwa Bora zaidi” amesisitiza Waziri Tabia