Waziri Lukuvi amaliza mgogoro wa ardhi Siha

0
177

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka Wananchi 288 wa kijiji cha Kilari wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, kuwalipa fidia Masista wa Shirika la Kazi wa Roho Mtakatifu wa Kanisa Katoliki katika eneo lenye ekari zaidi ya 200, ambalo Wananchi hao walivamia.

Akisuluhisha mgogoro huo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi amesema kila mwananchi atatakiwa kulipa shilingi elfu mbili kwa kila mita moja ya mraba kutokana na ukubwa wa eneo analo miliki.

Waziri Lukuvi amewataka Wakazi hao wawe wamemaliza kulipa fidia hiyo hadi ifikapo mwezi Mei mwaka 2021 na si vinginevyo.

Mgogoro huo wa ardhi kati ya Wakazi hao wa kijiji cha Kilari na Masista wa Shirika la Kazi wa Roho Mtakatifu wa Kanisa Katoliki umedumu kwa takribani miaka 40 sasa.

Nao baadhi ya Wananchi waliovamia eneo hilo wameishukuru Serikali kwa kumaliza mgogoro huo, na kuongeza kuwa kwa sasa wataweza kuendeleza maeneo yao.