Waziri Bashungwa na Naibu wake waitembelea TBC

0
410

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa wizara hiyo Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt Hassan Abbasi leo wametembelea Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo jijini Dar es salaam kwa lengo la kujionea utendaji kazi katika vitengo mbalimbali vya shirika hilo.

Katika ofisi za TBC I zilizopo eneo la Mikocheni, Viongozi hao wamepokelewa na mwenyeji wao Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayub Rioba na kutembelea vitengo mbalimbali, ambapo walipatiwa maelezo ya utendaji kazi wa kila siku katika vitengo hivyo.

Akiwa katika ofisi hizo za TBC, Waziri Bashungwa amewataka Wafanyakazi wa shirika hilo kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuifanya TBC kuendelea kuwa bora zaidi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Waziri Bashungwa na Naibu wake Ulega kuitembelea TBC, tangu walipoteuliwa na Rais Dkt John Magufuli kushika nyadhifa hizo.