Taasisi za Serikali zinazodaiwa na TANESCO kukatiwa umeme

0
215

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuwakatia umeme wadaiwa wote hata kama ni Taasisi za Serikali.

Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo jijini Dodoma alipokutana na viongozi wa wizara hiyo pamoja na wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara ya Nishari.

TANESCO inazidai Taasisi mbalimbali za Serikali zaidi ya Shilingi Bilioni 182 na Shilingi Bilioni 3.6 wanadaiwa wateja wa kawaida.

“Na nimeona tunadai zaidi Shilingi Bilioni 182 kwa taasisi za serikali, why?, tunawadai wateja wa kawada Shilingi Bilioni 3.6 kwa nini?, Mwenyekiti kwanza tunayemdai umeme kata umeme, acha nilaumiwe mimi kwanza kata tu,” amesisitiza Dkt. Kalemani.