Wanafunzi kuanza mitihani Jumatatu Zanzibar

0
221

Mitihani ya darasa la Nne, la Sita na kidato cha Pili Visiwani Zanzibar inatarajiwa kuanza Jumatatu Disemba 14.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, -Simai Mohamed Said amesema mtihani wa darasa la Nne utafanyika Disemba 14, wa darasa la Sita utaanza Disemba 17 hadi 21 na ule wa kidato cha Pili utaanza Disemba 22 hadi Disemba 31 mwaka huu.

Watahiniwa 50,217 wakiwemo Wasichana 24,688 na Wavulana 25,529 wameandikishwa kufanya mtihani wa darasa la nne.

Watahiniwa 34,029 wameandikishwa kufanya mtihani wa darasa la Sita na Watahiniwa 33,897 watafanya mtihani wa kidato cha Pili.