Nigeria kupokea chanjo dhidi ya Corona

0
201

Serikali ya Nigeria inafanya maandalizi kwa ajili ya kupokea dozi
milioni 20 za chanjo dhidi ya Corona, zijazotarajiwa kùwasili nchini humo mwanzoni mwa mwaka 2021.

Tangazo hilo limetolewa katika kipindi hiki ambacho wizara ya Afya ya nchi hiyo imeagiza kufunguliwa tena kwa vituo vilivyoandaliwa kwa ajili ya kuwatenga wagonjwa wa corona, baada ya kuwepo kwa taarifa za ongezeko la Wagomjwa hao.

Wizara ya Afya ya Nigeria imeeleza kuwa, kwa kuanzia chanjo hiyo itatolewa kwa Wafanyakazi wa sekta ya Afya na Wananchi wa hali za chini nchini humo.