Kanali Msumari afikisha bendera kileleni

0
157

Kanali wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Martin Msumari, amepandisha bendera ya Tanzania katika kilele cha mlima Kilimanjaro kilicho urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari.

Kanali Msumari amepandisha bendera hiyo akiwa na makundi ya watu mbalimbali wakiwemo Waandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Ahmed Salum na Silvanus Mauki, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika.

Akizungumza na TBC katika kilele cha mlima huo mrefu zaidi Barani Afrika na wa Pili kwa urefu duniani, Kanali Msumari amesema kupandishwa kwa bendera ya Tanzania katika kilele cha mlima Kilimanjaro ni ishara muhimu katika kuenzi mchnago wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kuhakikisha Tanganyika inakuwa huru.

Kwa mara ya kwanza bendera ya Tanzania ilipandishwa katika kilele cha mlima wa Kilimanjaro Disemba 9 mwaka 1964 na Kanali wa Jeshi la wananchi Alexender Nyirenda ikiwa ni ishara ya kuonesha Uhuru wa Tanzania

Kwa mwaka huu safari ya kupandisha bendera ya Tanzania katika kilele hicho ilianza Disemba 5.