Soko la madini latakiwa kuongeza mapato ya serikali

0
301

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge amelitaka Soko la Madini la Dar es salam kufanya kazi kwa weledi na makini ili kuongeza mapato ya serikali.

Kunenge ameyasema hayo leo Disemba 4, 2020 alipotembelea banda la Tume ya Madini katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo kunafanyika maonesho ya tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania.

Tume ya Madini inawakilishwa na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.