Mfanyabiashara mkubwa wa vyombo vya habari huko Hong Kong, Jimmy Lai amekataliwa dhamana katika mashtaka yanayomkabili ya udanganyifu na kutumia kinyume cha sheria eneo la kampuni yake.
Lai atatakiwa kuendelea kushikiliwa hadi mwezi Aprili mwakani kesi yake itakapoanza kusikilizwa.
Lai ambaye pia ni mwanaharakati amekamatwa baada ya kuanza kutumika kwa sheria mpya ya usalama, China imesema sheria hiyo mpya itarejesha hali ya utulivu.