Housegirl amchoma kisu mgeni

0
404

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP, Ramadhani Kingai amethibitisha kifo cha kijana aliyechomwa kisu na dada wa kazi.

Ezekiel Nyamko mkazi wa Kimara, alichomwa kisu mara mbili kwenye kifua na mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa rafiki yake, tukio lililopelekea kifo chake.

Kamanda Kingai ameeleza kuwa Nyamko alienda kumtembelea rafiki yake Kelvin ambaye wazazi wao pia ni marafiki na alipofika aliomba chakula lakini mtuhumiwa alimnyima na kumwambia kuwa bado wenyeji hawajala hivyo asubiri. Nyamko alimjibu kuwa “una roho mbaya kama sura yako” na kuongeza kuwa ndiyo maana Kelvin hamuoi.

Maneno hayo yalimkera mtuhumiwa na kufikia hatua ya kumchoma kisu kifuani mara mbili marehemu.

Mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Hapiness ameshikiliwa na polisi huku mwili wa marehemu ukiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi.