Makatibu Wakuu SADC -TROIKA wajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama

0
403
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiwasilisha mada katika Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya ushirikiano katika siasa, ulinzi na Usalama unaondelea Mjini Gaborone, Botswana

Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Mendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) -TROIKA wamekutana na kujadiliana mambo mbalimbali yakiwemo masala ya hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani ya SADC mjini Gaborone, Botswana.

Awali, Mkutano wa Makatibu Wakuu ulifunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Gaeimelwe Goitsemang ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.

Ni mara ya kwanza kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wa SADC kukutana ana kwa ana tangu ulipotokea ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (Covid-19).

Kwa upande wa makatibu wakuu waliohudhuria katika Mkutano huo kutoka Tanzania ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.

Mkutano wa Makatibu Wakuu utafuatiwa na Mkutano wa Dharua wa Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama baadae leo mchana mjini Gaborone.