Dkt. Abbasi: Waandishi tangulizeni uzalendo wa nchi

0
231

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amewahimiza waandishi wa habari kubadilika na kutanguliza uzalendo wa nchi kwanza wakati wa kuandika habari zao.

Dkt. Hassan Abbasi amesema hayo leo Novemba 17, 2020 wakati akifungua rasmi mkutano mkuu wa wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) mjini Morogoro.

Mkutano huo wa siku 2 ulianza Novemba 16, 2020 na unatarajiwa kumalizika leo.