Vunja Bei agawa vyombo kwa watumishi na wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili Taasisi ya Mifupa MOI

0
266

Shija Kamanija maarufu Vunja Bei ametoa zawadi ya vyombo kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika Taasisi ya Mifupa (MOI).

Huu umekuwa ni mwendelezo wa zoezi lake la kugawa vyombo katika taasisi za serikali na leo wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa MOI wamejipatia zawadi hizo

Vunja Bei amesema anasikia fahari kutoa zawadi kwa watumishi na wafanyakazi mbalimbali kwa kuwa wanajituma sana kutimiza wajibu wao na kuunga juhudi za Rais Dkt. John Magufuli katika kuwatumikia Watanzania

“Navitiwa Sana na uchapaji kazi wenu watumishi na wafanyakazi wa Serikali, na ndio maana kidogo ninachokipata nagawana nanyi ili kuwapa motisha” Vunja Bei ameeleza.

Vunja Bei amekuwa akigawa zawadi ya vyombo katika taasisi za serikali hasa katika sekta ya elimu, afya na jeshi la polisi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.