Donald Trump asema ameshinda uchaguzi Marekani

0
389

Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump amesema kuwa ameshinda uchaguzi mkuu, wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea nchini humo.

Katika hotuba aliyoitoa White House, Trump amekosoa vikali utaratibu wa kupiga kura katika uchaguzi huo wa urais kwa njia ya posta na kusema kuwa umepelekea wizi wa kura. Hata hivyo, Trump hakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo.

Viongozi mbalimbali wa kiasia nchini humo wamesema hatua hiyo haikubaliki, na si sahihi kimkakati na kusemwa na Rais wa nchi.

Awali alidai kuwa uchaguzi huo umekumbwa na kasoro nyingi na kwamba atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Katika uchaguzi huo, Rais Trump anachuana na mgombea wa Democratic, Joe Biden.