Ufaransa katika mapambano dhidi ya ugaidi Mali

0
261

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Florence Parly, amefanya ziara mjini Bamako, nchini Mali ambapo ameahidi kuwa Ufaransa itaendelea kushirikiana nao katika mapambano dhidi ya ugaidi.


Waziri Parly amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa mpito wa Mali Bah N’daw kuelezea mafanikio yaliyofikiwa na kikosi cha Barkhane, baada ya kuuwa wanamgambo Hamsini Kaskazini mwa Mali.


Amepongeza operesheni hiyo iliyofanywa kikosi cha Barkhane, ambacho pia kilikamata vifaa vya kundi hilo lenye mafungamano na Al-Qaeda.


Makao makuu ya jeshi la Ufaransa imesema kuwa operesheni hiyo ilifanyika karibu na mkoa wa Mali wa Boulikessi usiku wa Oktoba 30.