Watu 15 wafariki katika ajali Kagera

0
242

Watu 15 wamefariki dunia katika ajali ya gari mkoani Kagera leo, Kamanda wa Polisi, Revocatus Malimi amethibitisha.

Aidha, Kamanda Malimi amesema watu wengine 20 wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyohusisha basi la abiria la Emirate.

Uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea lakini taarifa za awali zinaonesha imetokana na hitilafu katika mfumo wa breki wa gari hilo.