Serikali kuendelea kumlinda mtoto wa kike

0
248

Serikali imesema itaendelea kusimamia na kuzilinda haki za watoto hususani mtoto wa kike dhidi ya madhila ya ukatili wa kijinsia.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. John Jingu wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Serikali imetunga sheria kali zinazomlinda mtoto wa kike dhidi ya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali watu wanaokiuka haki za watoto,” amesema Dkt. Jingu.

Pia emeongeza kuwa kumlea, kumtunza na kumlinda mtoto wa kike ni pamoja na kumpa haki yake ya msingi ya kupata elimu itakayomsaidia yeye na taifa lake.

Jamii isiyotengeneza watoto wake vizuri kesho yake itakuwa shida kubwa kwa taifa.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN Women), Hodan Addou amewataka wanawake kujitambua na kulinda haki zao ili kujenga taifa lenye usawa.

“Watoto wa kike ni wakati wenu kujitambua na kupaza sauti zenu ili haki yenu ya msingi isipotee.

Nao baadhi ya watoto waliohudhuria maadhimisho hayo wameipongeza serikali kwakuendelea kuweka misingi imara ya kuwalinda watoto dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.