Taifa Stars yaendelea kujinoa dhidi ya Burundi

0
449

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo Jumatano asubuhi kimeendelea na mazoezi yake ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi.

Mchezo huo utachezwa siku ya Jumapili, Oktoba 11, 2020 saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Stars imeingia kambini Oktoba 5, 2020 huku baadhi ya wachezaji wakitarajiwa kuwasili leo Jumatano wakitokea katika vilabu vyao.

Wachezaji hao ni pamoja na Himid Mao kutoka Misri, Simon Msuva, Nickosn Kababage kutoka Morocco.

Huku timu ya taifa ya Burundi ikitarajiwa kuwasili leo Jumatano na Ndege ya Air Tanzania wakiwa na msafara watu 32.