Siku ya Utalii Duniani: Tanzania mfano kuigwa katika utalii baada ya COVID-19

0
467

Leo Septemba 27, 2020 ni Siku ya Utalii Duniani, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe kama yale leo ikiwa na lengo la kuchochea shughuli za utalii duniani kote.

Maadhimisho ya mwaka 2020 yanaongozwa na kauli mbiu “Utalii na Maendeleo Vijijini”. Maadhimisho haya yanafanyika wakati ambapo janga la homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, linaendelea kuathiri sekta mbalimbali huku utalii ukiwa ni kati ya sekta ambazo zimeathirika sana.

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani zinaonesha kwamba, utalii kwa kipindi cha mwaka 2020 umepungua kwa kiasi cha watalii bilioni moja na hivyo kuifanya jumuiya ya kimataifa kupoteza kiasi kikubwa cha mapato sanjari na upotevu mkubwa wa nafasi za kazi.

Wakati hayo yakijiri maeneo mbalimbali, Tanzania tayari imefungua anga lake na kuruhusu shughuli za utalii ambapo watalii kutoka kote duniani wamekuwa wakifika nchi na kutembelea vivutio mbalimbali.

Shughuli za utalii zimerejea nchini Tanzania na hivi karibuni Taifa hilo la Africa Mashariki lilipata tuzo ya mhuri wa kimataifa kutokana na kuzingatia kanuni za kulinda wananchi na watalii.

Wadau mbalimbali wa utalii nchini wameipongeza serikali kwa kutofunga mipaka kama ambavyo nchi nyingi dunian zimefanya, lakini pia kwa kuweka mwongozo ambao unawawezesha kuendelea na shughuli zao za utalii kwa kuhakisha usalama wa wageni pamoja na wananchi.

Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za utalii ikiwemo ujangili serikali imeanzisha jeshi usu ambalo limekuwa likilinda na kutunza hifadhi mbalimbali.

“Mwaka 2014 katika hifadhi ya Mkomazi iliyoko mkoa wa Tanga na Kilimanjaro, idadi ya tembo ilipungua na kufikia 80 tu , lakini mwaka jana kwa muijbu wa takwimu tulizo nazo idadi imeongezeka na kufikia 1,200,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Bodinya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachia akizungumza na chombo cha habari cha Umoja wa Kimataifa.