RC Homera awajibu wanasiasa kuhusu uwanja wa Ndege Katavi

0
264

Serikali mkoani Katavi imethibitisha kuwa Uwanja wa Ndege wa Mpanda umekamilika kwa asilimia mia moja na unatumika tofauti na kauli za wanasiasa wanaosema uwanja umeota nyasi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amewahakikishia wananchi wa Tanzania na dunia kwa ujumla kuwa uwanja huo wa ndege ni miongoni mwa viwanja nchini vilivyokamilishwa kwa fedha ya walipa kodi iliyokusanywa katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano.

Homera amesema imefikia hatua kuwapuuza baadhi ya wanasiasa wanaowaaminisha wananchi wawapo katika majukwaa kuwadanganya kuwa Uwanja wa Ndege wa Mpanda uliojengwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda umeota nyasi na wanyama wa kufugwa wanakula.

Aidha, Homera ameendelea kuwapokea watalii kutoka mataifa mbalimbali wakiingia kwa kutumia usafiri wa anga kuja kutazama na kujionea vivutio vya utalii mkoani Katavi , hasa katika msimu huu ambao idadi ya watalii inaongezeka.