Nyota wa filamu ya Black Panther, Chadwick Boseman (T’challa) amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 43.
Taarifa ya kifo chake inaeleza kuwa Boseman alikuwa akisumbuliwa na saratani ya utumbo kwa kipindi kirefu huku akiendelea kuigiza filamu mbalimbali.
T’Challa amefariki akiwa nyumbani kwake huku amezungukwa na mkewe pamoja na wanafamilia wengine.