TCRA yaifungia Clouds TV na redio kwa kukiuka kanuni za uchaguzi

0
1160

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kukifungia kituo cha utangazaji cha Clouds TV na Clouds FM kwa muda wa siku saba kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 3 mwaka huu.

TCRA imechukua hatua hiyo kutokana na kituo hicho kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni za uchaguzi kupitia kipindi cha Clouds 360.

Aidha, TCRA imekitaka kituo hicho kusitisha matangazo kwa siku ya leo na kutumia muda uliobaki kuomba radhi kwa umma wa Tanzania.