Watu 70 wamekufa maji nchini Afghanistan

0
379

Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la Mashariki kaskazini mwa nchi ya Afghanistan, baada ya nchi hiyo kukumbwa na mafuriko makubwa yaliyokuwa yakiambatana na maporomoko ya udongo.

Hadi sasa watu sabini wamethibitika kufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea mafuriko mapya katika eneo hilo.

Uokoaji bado unaendelea nchini humo kwa tahadhari kubwa katika jimbo la Paiwan, hasa katika vifusi vya majengo yaliyoporomoka baada ya mafuriko hayo, kwani sauti za watu walionasa kwenye vifusi hivyo wakihitaji msaada zimeendelea kusikika.

Uongozi wa jimbo hilo unasema watu mbalimbali wamekuwa wakisaidia katika zoezi la uokoaji, lakini pia wameomba msaada kutoka katika serikali kuu.