Vijana tunapaswa kuchagua viongozi watakaosimamia maendeleo ya vijana na kutengeneza fursa kwa vijana ili kuleta ushindani wa kidiplomasia katika uchumi wa viwanda.
Hayo yamesemwa na mchambuzi wa masuala ya kidiplomasia, Goodluck Ng’ingo wakati akishiriki kongamano la Matarajio ya Vijana kwa Viongozi Wajao lililoandaliwa na TBC.
Ng’ingo ameongeza kuwa vijana wanapaswa kuepuka kutumika na watu wasioitakia mema nchi yetu katika masuala ya kisiasa ambapo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani na kuathiri uchumi wa Taifa.