RC Kunenge: Viongozi wa Dini mpo salama, msiwe na hofu

0
175

Askofu Zachary Kakobe amesema kuwa viongozi wa dini wameamua kuchagua upande kwa sababu Rais Magufuli amegusa dini kwa kiasi kikubwa sana.

Akitaja baadhi ya mambo amesema kuwa Tanzania imefungua ubalozi nchini Israel na nchini hiyo ina muwakilishi Tanzania.

Ameongeza kuwa, kwa zaidi ya miaka 40 wamekuwa wakiomba uchaguzi mkuu usifanyike siku za ibada, lakini haikufanikiwa hadi Rais Magufuli alipoingia madarakani na sasa uchaguzi utafanyika siku ya Jumatano.

Amesema pia, Rais Magufuli alikataa kufunga nyumba za ibada wakati wa janga la virusi vya corona, jambo liliwapa faraja sana. Lakini pia amekuwa akihusika kwenye shughuli zote bila kujadili dili wala dhehebu.