Hali ya tahadhari imetangazwa katika eneo la Jonglei, Sudan Kusini kufuatia mafuriko yaliyolikumba eneo hilo.
Habari kutoka Sudan Kusini zinasema watu kadhaa wamebaki bila makazi huku nyumba zaidi ya laki 5 zikiharibiwa na mafuriko hayo.
Serikali ya Sudan Kusini imesema msaada wa kibinadamu unahitajika kwa haraka kwa ajili ya watu walioathiriwa na mafuriko hayo.