NYATI MAJI: Aina ya Ng’ombe anaekaa kwenye maji

0
318

Kutokana na ukubwa wake, sura inayofanana na mnyamapori ‘Nyati’ na tabia ya kujilaza kwenye maji, Nyati Maji (Domestic Water Buffalo) amekuwa ni kivutio kwa wengi waliomuona.

Kama ilivyo Ng’ombe, Nyati Maji hufugwa nyumbani, nyama yake huliwa kama ilivyo ya ng’ombe ingawa tofauti ni moja, Nyati Maji huishi pia kwenye maji na ndio chanzo cha jina lake.

Akishashiba huingia ndani ya karo la maji lililojengwa bandani kwake na kujipumzisha.

Ally Mutabazi, Afisa Mifugo Msaidizi wa Mabuki Farms anapopatikana Nyati Maji, amesema kuwa mnyanma huyo ana asili ya Malaysia na ilikuwa ni zawadi kwa Hayati Baba wa Taifa kutoka kwa Rais wa nchi hiyo.

Nyati Maji huweza kufikisha hadi Kg1100 sawa na (tani 1.1)