Manara awatoa hofu wanasimba ishu ya Chama

0
387

Msemaji wa Mabigwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Kombe la FA, Haji Manara amewatoa hofu wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba SC kuhusu uvumi unaoendelea kuhusu kiungo wao Clatous Chama kujiunga na Yanga SC.

Manara amesema Chama bado ni mali ya Simba mpaka July 2021 hivyo wanasimba wasiwe na wasiwasi na uvumi huo.

“Chama ni mchezaji wa Simba mpaka 2021, tutaamua sisi kuongeza mkataba wake au vinginevyo. Ili aondoke timu nyingine sio Yanga tu timu yoyote ni lazima ilete barua ya kumhitaji ili tuwambie ofa yetu” alisema Manara.