Wasanii wa filamu watakiwa kuandaa filamu zenye ubora

0
330

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wasanii wa filamu nchini kufanya kazi zenye ubora na viwango vya juu ili kuboresha maslahi yao na kushindana na soko la nje .

Akizungumza na wadau wa filamu nchini wakati wa uzinduzi wa kanuni mpya za Bodi ya Filamu nchini, Waziri Mwakyembe amewataka wasanii kutumia maboresho ya kanuni hizo kwa kufanya kazi zenye ubora na viwango vya juu katika soko la ushindani.

“Ni wakati sasa kwa wasanii wa filamu nchini kufanya kazi nzuri kwani kanuni hizi zimepunguza tozo na ada mbalimbali kwa kiwango kikubwa lengo likiwa ni kumuwezesha msanii wa filamu nchini kufanya kazi katika mazingira mazuri,” amesema Waziri Dkt. Mwakyembe.