Afghanistan: Wafungwa 300 hawajulikani walipo

0
466

Msemaji wa Gavana wa Mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan anasema zaidi ya wafungwa 300 bado hawajulikani walipo baada ya shambulizi la kundi la kigaidi la IS katika gereza moja mjini Jalalabad.

Attaulah Khugyani amesema kuwa kati ya wafungwa 1,793, zaidi ya 1,025 walijaribu kutoroka ila wakakamatwa wakati wengine 430 walibakia ndani ya gereza hilo.

Msemaji huyo ameeleza kuwa watu 29 wamefariki dunia kutokana na makabiliano hayo na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.