Rais Mkapa alilipa hadhi zao la korosho

0
394

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Yusuf Nnanila amesema miongoni mwa mambo mengi ambayo Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa atakumbukwa kwayo ni pamoja na alivyoinua hadhi ya zao la korosho.

Nnanila ameyasema hayo wakati akizungumza na TBC akiwa msibani Lupaso, nyumbani kwa Rais Mkapa ambapo ndipo maziko yatakapofanyika kesho.

Amesema Mzee Mkapa alipanua ulimaji wa zao la korosho kutoka mikoa mitano aliyoikuta hadi mikoa 17 wakati anatoka madarakani.

Aidha, amesema Mkapa ndiye aliyeanzisha mfumo wa Stakabadhi Ghalani unaotumiwa na wakulima hadi sasa kuuza mazao yao. Ameongeza kuwa kiongozi huyo aliweza kupandisha bei ya korosha hadi kufikia shilingi 3,000 kwa kilo moja.

Amesema mbali na Mkapa kuwa chachu ya maendeleo kwa mikoa ya kusini hasa kwa ujenzi wa daraja katika Mto Rufiji, alikuwa mlezi wa kisiasa wa watu wengi ambao walitegemea ushauri wake na alitoa ushirikiano kila alipohitajika.