Mambo matatu nitakayomkumbaka nayo Rais Mkapa.

0
203

“Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amefanya mambo mengi, lakini mimi, Askofu Angelus Mchomanjoma wa Kanisa la Sayuni International Pentecote, (Masasi) Tanzania nitamkumbuka kwa haya matatu;

  1. Ujenzi wa daraja katika Mto Rufiji (Daraja la Mkapa). Safari ya Masasi, Mtwara hadi Dar es Salaam ilikuwa inachukua hadi siku saba, lakini daraja lile limerahisisha usafiri.
  2. Ujenzi wa shule za msingi nchi nzima. Hili limethibitisha uzalendo wake.
  3. Aliposema ‘mimi sio Rais wa Masasi.’ Watu wa Masasi walilipokea hili kwa namna isiyoelezeka, lakini sasa tunaona umuhimu wake.

Mzee Mkapa kwa kuwa Rais alitakiwa ajipendelee, lakini hakufanya hivyo, wazee walipomuendea kuhusu matatizo ya Masasi, alisema ‘Mimi si Rais wa Masasi, ni Rais wa Tanzania.'”