Vijana wa Lusapo wanavyomfahamu Mkapa

0
187

Baadhi ya vijana ambao ni wakazi wa Kijiji cha Lupaso, wilayani Masasi Mkoani Mtwara wamesema kuwa wanamfahamu Marehemu Rais Benjamin Mkapa kama mzalendo wa kweli.

Vijana hao wamesema kiongozi huyo kila mara alipokuwa akija nyumbani (Lupaso) alikuwa akiwaalika wote bila ubaguzi na kushiriki nao katika chakula na mazungumzo mbalimbali.

Aidha, wameeleza kuguswa na msiba huo, lakini wamesema itabaki kuwa fahari kwa Kijiji cha Lupaso kutoa Rais wa Tanzania.