Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ameagiza wasimamizi wa uchaguzi ndani ya chama hicho kuhesabu kura zote mbele ya wajumbe wa mikutano.
Akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma Rais Magufuli amesema kama ilivyofanyika kwenye vikao vya kutafuta wagombea wa Urais, kura zihesabiwe mbele ya wajumbe ili kila mmoja ajue kwa uwazi amepata nini.
“Kura zikishamaliza kupigwa, zikafanyiwe kama tulivyofanya kwenye Halamshauri Kuu, zihesabiwe hadharani. Anayepa zero [sifuri] apate hapo hapo na anayepata zote apate pale pale, na huu uwazi utaendelea kujenga kujenga umoja wa sisi wana-CCM,” amesema Rais.
Mchakato wa kura za maoni umeanza leo kwenye mikutano ya majimbo ambapo zoezi hilo litamalizika kesho Julai 21, 2020.
Akizungumzia idadi ya watia nia wa chama hicho katika ngazi ya ubunge na uwakilishi nchi nzima, Rais Magufuli amesema watia nia ni 10,367 huku waliorejesha foimu wakiwa ni10,321.