Rais Magufuli: Sijamtuma mtu kugombea ubunge

0
445

Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi amesema kuwa hadi Julai 16, 2020 asubuhi zaidi ya wanachama 8,000 wa chama hicho walikuwa wametia nia ya kugombea ubunge.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni ambapo ameeleza Mkoa wa Dar es Salaam ndio unaongoza ukiwa na jumla ya watia nia 829.

Aidha, Rais Magufuli ametumia wasaa huo kusisitiza kuwa taarifa kwamba baadhi ya watia nia wametumwa na viongozi wa serikali na chama akiwemo yeye na viongozi wengine wakiwemo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Makamu Mwenyekiti wa CCM au Katibu Mkuu wa CCM na viongozi wa vyombo vya ulinzi si za kweli.

Ametaka chama hicho kuwapima watia nia wote kwa usawa na kwamba wao hawajamtuma mtu, bali wanataka wananchi wachague wenyewe wa kumtuma.

Hata hivyo amesema uwepo wa idadi hiyo kubwa ya watia nia ni ishara ya kukomaa kwa demokrasia ndani ya chama hicho.