Wapiganaji wa Houthi wafanya mauaji Saudia

0
489

Wapiganaji wa kikundi cha Houthi cha nchini Yemen wamedai kuwaua maafisa kadhaa wa jeshi la Saudi Arabia, baada ya kufanya mashambulio ya anga nchini humo.

Wapiganaji hao wamedai kufanya mashambulio kadhaa nchini Saudi Arabia hasa katika maeneo ya mpakani na kulenga visima vya mafuta ambavyo navyo vimelipuka.

Serikali ya Saudi Arabia imesema majeshi yake yalifanikiwa kudaka makombora kadhaa yaliyorushwa na wapiganaji hao wa kikundi cha Houthi na kufanikiwa kuzinasa ndege kadhaa zisizokuwa na rubani usiku wa kuamkia hii leo.

Hata hivyo Saudi Arabia haijasema kama kuna mtu aliyeuawa ama kujeruhiwa katika tukio hilo.