COSOTA sasa kuhamia wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

0
330

“Ninafahamu nina deni kubwa kwa Wasanii kuhusu kubadili shughuli za Wasanii kutoka wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Sanaa, mnaita COSOTA imesota sana huko, nawaahidi Wasanii kabla ya kufika Jumapili inayofuata haya yote nitayamaliza,
Waziri Mwakyembe nataka kabla haujaenda kuchukua fomu kule kwenu uje uchukue barua nitakayokuwa nimeisaini ya kuhamisha shughuli za COSOTA kutoka kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara kuja kwenye wizara yako ili hawa vijana wafaidike na usanii wao”, Rais Magufuli.

Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ametoa kauli hiyo jijini Dodoma katika hafla ya chakula cha mchana aliyoiandaa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM iliyofanyika Ikulu ya Chamwino.