Rais Magufuli ateua Mkurugenzi mpya Kituo cha Uwekezaji

0
771

Rais John Magufuli amemteua Dkt. Maduhu Kazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kazi alikuwa Meneja wa Idara ya Sera za Kibajeti na Madeni wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Dkt. Kazi anachukua nafasi ya Godffrey Mwambe.

Uteuzi wa Dkt. Kazi unaanza leo Julai 12, 2020.